Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Israel imeshambulia maeneo ndani ya ardhi ya Syria mara tatu mapema leo Jumanne kwa ndege za kivita pamoja na makombora na mizinga , limesema jeshi la Syria katika taarifa iliyotangazwa na televisheni ya taifa.
Ndege za jeshi la Israel zimeshambulia eneo la Qutayfeh kaskazini mashariki mwa mji mkuu Damascus , na makombora yaliangukia karibu na maeneo ya kijeshi na kusababisha jeshi la Syria kujibu mashambulizi na kuijeruhi ndege ya kivita ya Israel.
Israel pia ilifanya mashambulio ya makombora ya ardhini ndani ya Syria kutoka katika eneo linalokaliwa na Israel la milima ya Golan, lakini jeshi la Syria limeyazuia makombora hayo, na kushambulia vikali kambi za jeshi za Israel.
Taarifa ilisema kwamba ndege za jeshi la Israel baada ya kushindwa kuingia Syria zilishambulia tena kwa mara ya mwisho kwa maroketi manne kutoka ndani ya Israel, na kwamba mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria ulifanikiwa kuangusha baadhi ya makombora hayo.
Jeshi la Syria limesema mfumo wa kulinda anga umefanikiwa kuangusha baaadhi ya makombora hayo na mengine yaliangukia katika moja kati ya maeneo ya kijeshi ya syria, na kusababisha uharibifu wa mali.
Mwisho wa uchokozi wa Israel umewadia
Jeshi la Israel limekuwa likifanya mashambulizi mara kwa mara dhidi ya jeshi la Syria na washirika wake wa Lebanon, wa kundi la Washia la Hezbollah tangu mwanzo wa mzozo wa ndani wa Syria mwaka 2011. Ambapo jeshi la Israel limekuwa likiyasaidia makundi ya kigaidi yanayopambana na serikali ya Syria.
Msemaji wa jeshi la Israel alikataa kuelezea lolote kuhusiana na taarifa iliyotolewa na Syria. Licha ya kuwa mkuu wa jeshi la Israel mwezi Agosti mwaka jana alisema kwamba wanajeshi wake waliishambulia Syria karibu mara 100, sera za Israel kwa jumla ni kutothibitisha ama kukataa operesheni kama hizo.
Israel imeapa kuizuwia Iran kutumia ardhi ya Syria kuweka vituo vyake vya kijeshi ama kupitishia silaha nzito kwenda kwa kundi la Hezbollah nchini Lebanon, kundi ambalo limekuwa likisaidia Syria katika vita vyake dhidi ya magaidi wanaodhaminiwa na Marekanina washirka wake vilivyodumu kwa miaka saba huku jeshi la Syria likionyesha mafanikio.
Katika taarifa yake jeshi la Syria imetoa onyo kabla la kulipiza kisasi kwa mashambulizi hayo ya anga na kubainisha kuwa Israel inaendelea kuyasaidia makundi yakigaidi nchini Syria. maba
Israel ilikamata kilometa 1,200 za milima ya Golan kutoka Syria katika vita vya siku sita vya mwaka 1967 na baadaye kulichukua kabisa eneo hilo katika hatua ambayo haijatambuliwa na jumuiya ya kimataifa. Syria na Israel zinaendelea kuwa katika hali ya kivita, na taifa hilo la Kiyahudi lilipigana vita vikali dhidi ya Hezbollah mwaka 2006 ambapo majeshi ya Israel yalilazimika kusalimu amri kwa mara ya kwanza.
Majeshi ya Iran kwasasa yapo nchini Syria na yanaendelea na kazi za kuyaangamiza makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Marekani, Israel na washirika wao, uwepo wa majeshi ya Iran nchini Syria ni hatari kubwa kwa usalama wa Israel.
Majeshi ya Iran yamesema yatazisaidia Syria, Palestina na Lebanon kurudisha ardhi zao na kupambana na Israel mpaka mwisho wa taifa la Israel.
Mwisho wa habari / 291